HIVI MORRISON ANA KIPI CHA ZIADA?
BAADA ya kurejea kikosini, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison ameonekana kupewa mazoezi maalum ya kufunga huku ikielezwa ni kwa ajili ya kuiua Simba. Morrison ambaye kwa siku za karibuni alikuwa na mgogoro na mabosi wake kiasi cha kutolewa kwenye timu, juzi aliungana na wenzake mkoani Kagera ambapo jana Jumatano walicheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, huku yeye akianza kikosi cha kwanza na kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0. Mghana huyo ambaye alipeleka kilio katika mchezo uliopita walipokutana Yanga na Simba kwa bao lake la faulo ya moja kwa moja dakika ya 44 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara, kocha wake, Mbelgiji, Luc Eymael tayari amemuweka kwenye mipango yake. Katika mipango hiyo, ameonekana kumpa mazoezi maalum ya kufunga kumuandaa na mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Simba ukiwa ni wa nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar kuanzia saa 11:00 jioni. Taarifa kutoka katika kambi ya Yanga iliyop...