Posts

Showing posts from July, 2020

HIVI MORRISON ANA KIPI CHA ZIADA?

Image
BAADA ya kurejea kikosini, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison ameonekana kupewa mazoezi maalum ya kufunga huku ikielezwa ni kwa ajili ya kuiua Simba. Morrison ambaye kwa siku za karibuni alikuwa na mgogoro na mabosi wake kiasi cha kutolewa kwenye timu, juzi aliungana na wenzake mkoani Kagera ambapo jana Jumatano walicheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, huku yeye akianza kikosi cha kwanza na kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0. Mghana huyo ambaye alipeleka kilio katika mchezo uliopita walipokutana Yanga na Simba kwa bao lake la faulo ya moja kwa moja dakika ya 44 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara, kocha wake, Mbelgiji, Luc Eymael tayari amemuweka kwenye mipango yake. Katika mipango hiyo, ameonekana kumpa mazoezi maalum ya kufunga kumuandaa na mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Simba ukiwa ni wa nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar kuanzia saa 11:00 jioni. Taarifa kutoka katika kambi ya Yanga iliyop...

CHINA YAIKOSOA MAREKANI

Image
Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema kitendo cha Marekani kujitoa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ni pigo kubwa, Spahn ameandika kwenye ukurasa wa Twitter kuwa kujitoa kwa Marekani kutoka WHO ni pigo kubwa kwa ushirikiano wa Kimataifa, na kutoa wito wa ushirikiano zaidi kupambana na majanga. Waziri huyo ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya utapendekeza mageuzi kuifanya WHO kuwa imara zaidi. China pia imeikosoa Marekani kwa kujitoa kutoka shirika hilo na kusema hatua hiyo itakuwa na athari mbya kwa Mataifa yanayoendelea. Marekani imemfahamisha rasmi jana Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusiana na Nchi hiyo kujitoa WHO kwa madai Shirika hilo limeshindwa kupambana na corona na linaipendelea China.

BEI ELEKEZI YA UMEME KWA MATUMIZI YA KAWAIDA

Image
Waziri wa Nishati, Dkt.  Medard Kalemani , ametoa onyo kali kwa wazalishaji binafsi wa umeme, wanaowatoza wananchi gharama kubwa tofauti na bei elekezi. Waziri amesema gharama ya umeme kwa wananchi wenye matumizi ya kawaida ni Tsh. 100 kwa unit moja. Alisema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kahunda, Wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza. Alitoa agizo kwa viongozi wa Serikali, kuwachukulia hatua wazalishaji binafsi wa umeme, watakaobainika kukiuka agizo hilo. Alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi, hasa wanaoishi visiwani hivyo Serikali haitavumilia tabia za baadhi ya wawekezaji binafsi kwani imewaamini kutenda haki katika kuwafikishia umeme wananchi ambao hawajafikiwa na Gridi ya Taifa. Waziri aliagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa wawakilishi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa Jua ya Jumeme, baada ya wananchi wa kisiwa cha Maisome kuwatuhumu kuwauzia umeme kwa Tsh. 3,500 kwa unit moja.

WEMA AKIRI

Image
STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema kuwa anajijua kuwa ana miguu mibaya, lakini hiyo isiwafanye watu kuwa ndiyo fimbo ya kumchapia. Akizungumza na Risasi Vibes, mrembo huyo alisema kwamba hakuna binadamu mkamilifu hapa duniani na Mungu hawezi kukupa vyote, hivyo yeye amekubali kunyimwa miguu mizuri. “Unajua nimechoka na maneno ya watu wa mitandaoni, kila siku wanakesha kuisema vibaya miguu yangu, ukute ya kwao ni mibaya yangu ina afadhali, halafu Mungu hakupi vyote, lazima kuna ambacho atakunyima ili na wengine wapate, ndivyo alivyofanya kwangu, najua nina miguu mibaya, ila sitaki kuendelea kusemwa,” alisema Wema. STORI | Memorise Richard

Waziri Mkuu Afariki Dunia Baada ya Mawaziri Kukutana

Image
WAZIRI Mkuu wa Ivory Coast, Amadou Coulibaly, amefariki dunia jana Jumatano, Julai 8, 2020, jijini Abidjan ikiwa ni muda mfupi baada ya kuugua wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri la nchi hiyo na alikuwa amerejea hivi karibuni kutoka nchini Ufaransa kwa ajili ya matibabu ya moyo kwa miezi miwili. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61 aliyezaliwa Februari 10, 1959, alikuwa amechaguliwa kuwa mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa mwezi Oktoba,mwaka huu baada ya Alessane Ouattara kusema kuwa hatowania tena muhula wa tatu. Rais Ouattara ametangaza maombolezo ya kitaifa ya msiba huo huku akieleza kwamba Coulibaly alianza kuhisi vibaya wakati wa kikao cha kila wiki cha baraza la mawaziri na akapelekwa hospitali ambapo alifariki baadaye na kuwa kifo chake kitasababisha hali ya sintofahamu kuhusu uchaguzi huo. Coulibali alifanyiwa upandikizaji wa moyo mwaka  2012 na alikuwa alikwenda Ufaransa Mei 2, 2020, ili kuwekewa bomba katika mshipa wake wa damu. Alirejea nchini k...

Simba Yatuma Salamu Yanga

Image
BAADA ya Simba jana kutoka 0-0 na Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, ilikabidhiwa kombe kutokana na kuwa mabingwa wa ligi hiyo msimu huu.Baada ya kukabidhiwa kombe hilo, wakawa wanatamba wakiwaambia Yanga kwamba: “Hamtuwezi, tukikutana Jumapili tunawachapa na msimu ujao katika ligi tunakuwa tena mabingwa. ”Mchezo huo wa jana Simba ilikuwa inahitaji heshima kwa kuwa imeshamaliza kazi ya kutwaa ubingwa, huku Namungo FC ikihitaji kuongeza mbio za kubaki ndani ya tano bora. Simba iliyokuwa ikimtumia mshambuliaji wake namba moja Meddie Kagere mwenye mabao 19, alishindwa kufurukuta mbele ya mikono ya Nurdin Barola ambaye alikaa imara kwenye lango lake. Kipa wa Simba, Beno Kakolanya alianza jana ikiwa ni mchezo wake wa nane ndani ya Ligi Kuu Bara chini ya Sven Vandenbroeck alifanikiwa kuokoa hatari za Bigirimana Blaise ambaye alitolewa kwa ulazima dakika ya 40 baada ya kupata majeraha. Matokeo hayo ya jana yameifanya Simba...

Mwanamke Shujaa aliyemuokoa Mtoto nyumba ikiwaka moto, mwenyewe afariki

Image
Hii video imewasikitisha wengi walioitazama ambapo pamoja na kuhuzunisha, Mwanamke huyu aliyemrusha mwanae kupitia kibarazani ametajwa na wengi kama shujaa, ni tukio la moto kuunguza nyumba gorofa ya tatu huko Phoenix, Arizona Marekani ambapo inaripotiwa ndani ya nyumba alikuwepo Mama na Mtoto na kwenye hii video Mama anaonekana akimuokoa Mtoto wake kwa kumrusha chini kupitia kibarazani. Kwa mujibu wa  ABC NEWS , Mama huyo alifariki kwakuwa alikua ameungua sana lakini alipambana na kuhakikisha amefika kibarazani na kumrusha Mtoto wake chini ambapo alidakwa na Watu wawili kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini, Mungu amlaze pema. (tahadhari video inaogofya)

Kauli 7 za Joshua Nassari baada ya kujiunga na CCM Jana

Image
Joshua Nassari  aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa ticket ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo July 8 2020 kwenye ukumbi wa CCM Arusha ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM ambapo hizi hapa chini ni kauli zake saba miongoni mwa mengi aliyoyazungumza ambayo unaweza kuyatazama zaidi kwenye video mwishoni mwa hizi kauli. “Wengine wanasema Nassari anautaka Ubunge, niwaambie sijatangaza nia mahali popote na sijaja CCM kutangaza nia, nimetafakari na pia Jamii, Wazee wa Meru na Marafiki waliofanya nikawa Mbunge mdogo kuliko wote Nchi hii wameniambia, naona CCM huku kunafaa” “Haikuwa kazi rahisi kufanya haya maamuzi ya kuja CCM, yale yote mnayotaka kuyasikia na kuyaona kutoka kwangu mtayasikia na kuyaona hata kama sio leo, sababu kubwa iliyonileta CCM ni kwakuwa naipenda Nchi yangu” “Ukiongea habari ya Ndege.. Wapingaji wanasema nani anapanda? mbona wakati wa Mwl. Nyerere hamkusema Mwl. unatupa Ndege hatuna hela ya kupanda, leo tuna Ndege 11, ile...

MSANII GIGY MONEU KURUDI SHULE

Image
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amesema kwamba, ameamua kurudi shule ili atimize malengo yake ambayo hakuweza kuyatimiza nyuma. Akipiga stori mbili tatu na Risasi Vibes, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake, alisema kwamba siku nyingi alikuwa anafikiria kurudi shule, ila alikuwa anaweka sawa baadhi ya mambo na sasa kila kitu kipo vizuri. “Nimerudi shule na sasa naingia masomo ya jioni, nitakuwa nasomea mambo ya sheria kwa sababu ndiyo kitu ninachokipenda,” alisema Gigy. STORI Memorise Richard,

EBU IELEWE VYEMA MIAKA 5 YA RAIS WETU MAGUFULI,

Image
MKURUGENZI wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC), Geoffrey Mwambe amesema kuwa Miundombinu iliyojengwa na Serikali imewezesha kituo hicho kupiga hatua kubwa na kulete wawekezaji wengi katika Sekta ya uwekezaji hasa kwenye sekta ya Viwanda. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mwambe amesema miundimbinu iliyojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kipindi hiki cha miaka mitano imekuwa ni mishipa ya kituo hicho kufanikisha sekta hiyo muhimu nchini. “Miundombinu iliyojengwa na Serikali kwenye hii miaka mitano sisi kwetu kama kituo cha uwekezaji inatumika kama mishipa ya damu, kwani inapunguza gharama ya usafirishaji, kwa hiyo imetusaidia ndani ya miaka hii mitano ya Rais Magufuli tokea Juni 2016 hadi Juni 2020 tumeweza kusajili miradi 1, 312 yenye thamani ya dola za Kimarekani Bilioni 20”, Alisema Mwambe. Alibainisha kuwa asilimia 54 ya miradi hiyo ipo sekta ya viwanda ambayo imeisaidia Tanzania kuingia...