BEKI wa kulia Mtanzania, Hassan Kessy, anayekipiga Nkana FC ya Zambia, amesema yupo tayari kurejea Yanga kwa dau la Sh milioni 80. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu zizagae tetesi za beki huyo kutakiwa na Yanga baada ya mkataba wake na Nkana kutarajiwa kumalizika Julai, mwaka huu. Yanga imepanga kuiboresha safu yao ya ulinzi hasa upande wa kulia baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Luc Eymael kutoa mapendekezo ya kusajiliwa beki mwingine na jina la Kessy kupitishwa.Akizungumza na Spoti Xtra, Kessy alisema aliondoka Yanga vizuri bila ya kugombana na ungozi, wachezaji na mashabiki, hivyo yupo tayari kurejea kuichezea timu hiyo kwa moyo mmoja. “Nimeichezea Yanga kwa mafanikio makubwa na kati ya hayo ni kuipa ubingwa wa ligi msimu wa 2016/2017. “Nitakuwa tayari kurejea Yanga kwa makubaliano maalum, kikubwa ninachokiangalia ni maslahi, hivyo nitasaini kwa dau la Sh milioni 80. Tayari klabu yangu ya Nkana imenipa ofa ya kuongeza mkataba mwingine wa kuendelea kubaki,” ali...